Namna ya kufungua akaunti ya Play Store kwa kutumia anuani ya barua pepe ya Gmail iliyokwisha kutengenezwa zamani
- Washa simu yako
- Hakikisha una kifurushi cha intaneti
- Hakikisha simu yako umeifanyia Internet Configuration na signals za data zinasoma
- Washa Mobile Data
- Fungua Programu ya Play Store
- Kwenye Sehemu ya Add a Play Store Accountchagua Existing.
- Ingiza anuani ya barua pepe pamoja na neno lako la siri kisha bofya kitufe cha kuendelea (Next/Continue)
- Kwenye Sehemu ya “Set up payment info” bofya ‘SKIP’
- Kwenye Backup and restore bofya kwenye kisanduku cha Keep this phone backed up with my Google Account Kisha bofya kitufe cha kuendelea (Next/Continue)
- Ukikutana na ujumbe unakuomba ukubaliane na masharti ya kutumia huduma za Play Store utabofya kwenye Accept, na hapo akaunti yako itakuwa tayari.
Zifuatazo ni hatua za kutengeneza akaunti mpya ya Google na Play Store kwa wakati mmoja:
- Washa simu yako
- Hakikisha una kifurushi cha intaneti
- Hakikisha simu yako umeifanyia Internet Configuration na signals za data zinasoma
- Washa Mobile Data
- Fungua Pogramu ya Play Store
- Kwenye Sehemu ya Add a Play Store Accountchagua New.
- Jaza Jina la kwanza na la mwisho kisha bofya kitufe cha kuendelea (Next/Continue)
- Ingiza anuani ya barua pepe kisha bofya kitufe cha kuendelea (Next/Continue)
- Ingiza na rudia kuingiza neno la siri kisha bofya kitufe cha kuendelea (Next/Continue)
- Kwenye Sehemu ya “Set up payment info” bofya ‘SKIP’
- Kwenye Backup and restore bofya kwenye kisanduku cha Keep this phone backed up with my Google Account Kisha bofya kitufe cha kuendelea (Next/Continue)
- Ukikutana na ujumbe unakuomba ukubaliane na masharti ya kutumia huduma za Play Store utabofya kwenye Accept
Baada ya kufanya yote hayo ya juu programu ya Play Store itakuwa tayari na itakupa nafasi ya kutafuta na kupakua programu, michezo ya simu (mobile games) pamoja na muvi mbalimbali.
Comments
Post a Comment